UJUMBE MAALUM KUTOKA KWA Mch. TED WILSON
RAIS WA KONFERENSI KUU LA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO (GENERAL CONFERENCE)

Ninayo furaha sana kukutana nani juma hili, Ndiyo na nyie wapendwa waumini wa Kanisa duniani kote. Mungu ameweza kuilinda na kuitunza Kanisa lake. Ni kwa Neema ya Mungu mmelindwa juma hili. Hivyo kuwa mtu wa tumaini katika Bwana, Ni hakika tutashinda (tuavuka) salama katika hili.
Na mnayo nafasi kama TMI (Total Member Involvement) kushiriki/kuhusiana na watu kwa kutumia Barakoa yako, kukaa katika umbali unaopendekezwa. Lakini Yawezekana kuna muumini/ babu au bibi ambaye hawezi kupata chakula, waweza kumsaidia: yawezekana pia Yupo mtu fulani ambaye anahitaji  Barakoa na unajua pa kuzipata, waweza pia kumsaidia. Yaewezekana pia kuna wale ambao wanahitaji  fulani maalum na kwa namna fulani unaweza kuwatia moyo. Ebu angalau wapigie hata simu na kuwapa maneno ya faraja kuwa "Hakika tutapita katika hili kwa rehema za Mungu". Na unapofanya hivyo unaweza kutangaza ujumbe wa malaika watatu. Unapowavuta na kuwaelekeza watu katika Neno la Mungu hususani "Ufunuo 14", kusaidia watu kuelewa kwamba Yesu anakuja upesi. Hata kama tutapitia changamoto za kiuchumi, au hata changamoto za sasa za kukosa kazi Mungu atamsaidia kila mmoja wetu.

Nataka nishiriki na wewe maneno mazuri ya Mungu katika kitabu cha Zaburi 34: 4-7 kidogo tu. Hili ni jambo ambalo linaweza kukonga moyo wa kila mmoja wetu. Ni jambo jema kiasi gani kumuomba Mungu atulinde tunapokabiliana na nyakati ngumu mbele yetu? Na ni nafasi kubwa zaidi kiasi gani kuweza kushiriki maneno ya Mungu na habari njema za ujio wa Yesu Kristo upesi..?

Tuangalie, Zaburi 34:4-6 "Nalimtafuta Bwana akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote. Wakamwelekea macho wakatiwa nuru, Wala nyuso zao hazitaona haya. Maskini huyu aliita, Bwana akasikia, Akamwokoa na taabu zake zote". Unaweza kuamini kuwa Bwana atakusiki? Wakati mwingine hajibu kwa namna unavyotaka Lakini tambua anakusikia na atakujibu katika wakati sahihi. Woga waweza kuwa nao juu ya kesho yako, juu ya wanaokuzunguka n.k Lakini Mungu anaweza kukusaidia na kukufanya uwatie moyo wengine. Mwenye kuondoa woga ni Yesu Kristo. Utashangazwa, unapojazwa na Roho Mtakatifu maana kila wakati utakuwa Nuru.
Taabu yote na changamoto zote tunazokumbana nazo, majanga yote na shida zote tunazopitia, tukiweka mikono yetu katika mikono  ya Yesu Hakika atatuokoa. Katika kitabu cha Zaburi 34:7 tunayomslizia ambayo ni burudiko na faraja ya moyo na yawezekana tumeikariri inasema, " Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa".
Ni nafasi nzuri ilioje kuwa sehemu ya mtoto wa Mungu unapotambua jinsi anavyokulinda, kukutetea, kutusaidia na kutuokoa. Yapo maneno katika kitabu cha Ellen G. White cha Wazee na Manabii uk 290 yakisema " Mara nyingi maisha ya Mkristo yanagubikwa na hatari, na kazi zinaoneonekana kuwa ngumu kufanyika......Hata hivyo sauti ya Mungu inadumu kusema kwa umakini kabisa kwamba, Endelea Mbele. Hebu na tutii sheria za Mungu hata Kama macho yetu hayawezi kupenyeza giza...."https://youtu.be/ZjQ57PRW8As:



Comments

Popular posts from this blog

KALENDA RASMI YA MATUKIO YA KANISA - SEC 2020