TUMAINI KATIKA UPEO WA MACHO Biblia imejaa matumaini. Mtume Paulo hasa ni mtume wa matumaini. Anaandika kwa kanisa la Rumi, anawatia moyo kwa maneno haya, "kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi, ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini" Warumi 15:4. Sura ya 15 inahitimisha na maneno haya: " Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu". Wakati siku zijazo zinapoonekana kuwa na mashaka, Neno la Mungu hujaza mioyo yetu kwa tumaini. Paulo akimwandikia Tito katika Tito 2:13 anamthibitishia kudumu " ukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na mwokozi wetu. Historia ilikuwa na mahali pa kuanzia na itakuwa na mahali pa kuishia. Ilianza Mungu alipoimba dunia hii, na upeo wa uumbaji ni kurudi kwa Bwana wetu, ambaye hatimaye ataumba upya mbingu mpya na nchi mpya. Kuna m...