SAFINA NDANI YA SAFINA YA KWELI.
Na. Mch Filbert Joseph Mwanga
Fungu kuu: Mwanzo 6:14
Wimbo No: 107
Kanisa la Mungu ndiyo SAFINA ya hapa duniani inayotuongoza kuifikia SAFINA ya kweli ya mbinguni.
Ndani ya Kanisa lipo Idara ya Shule ya Sabato ambayo ndio Moyo wa kanisa unaodunda barabara. Tusiposimamia Idara hii vyema basi haitadunda barabara.
Mwanzo wa machukizo yalianza kipindi cha Nuhu wakati wana wa Mungu walipo anza kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Mwanzo 6:1,2...inaelezea
Ndoa za mseto zikaongezeka, kilikuwa kipindi cha uasi, hawakujua kuwa Mungu ndiye aliwaumba.
Wana wa Mungu ni wale pekee wanaomtii Mungu kupitia sheria zake.
Kumbukumbu la Torati 14:1... Inaelezea zaidi juu ya wana wa Mungu.
Yohana 1: 12; inasema wote waliompokea Bwana (Yesu Kristo) yeye huyo Yesu aliwafanya kuwa watoto wa Mungu.
Kaini baada ya kufanya dhambi ya kumuua ndugu yake (Habili) watoto wake hawakuitwa Shetani bali ndio tunaambiwa katika kitabu cha Mwanzo 6: 1,2 kuwa ni wana wa wanadamu, watoto wa Sethi ndio walioitwa wana wa Mungu.
Hivyo tafauti kati ya haya makundi mawili ni kuwa: wana wa Mungu ni wale wanaokubali kutii Sauti ya Mungu na imani ya Yesu. Watu wa Mungu ni wale wote wanaoendelea katika kutenda maovu (hawaitwi shetani)
Katika kanisa la Mungu yapo makundi mawili tunapaswa kuwatambua ili kujua namna ya kuenda nao. Mfano wa watu wenye Pressure; wenye pressure ya chini; yaani hawa ni wale ambao wanaona kila kitu kwao ni sawa mfano 1. Aje amechelewa kanisani, 2. Atoe zaka (akitoa au asipotoa yeye kwake ni sawa), 3. Asome Biblia au lesoni au asivisome yeye kwake anaona ni sawa.
Kundi lingine ni mfano wa wale wenye pressure ya juu; hao ni wale ambao hawapendi/hawawezi kufanya mambo kwa utulivu na badala yake wanafanya mambo kwa kuhamaki kwamfano; ni watu wanaopenda kukosoa tu mambo, kila kitu yeye kwake anaona limekosewa.
Mfano wa SAFINA ni ubatizo wa kweli 1Petro 3:20,21 inaelezea juu ya hilo.
Ndoa zipo za aina nyingi ambazo watu wa Mungu wameweza kufunga ambayo ni machukizo kwa Mungu. Mikataba na wa nje katika biashara ni ndoa, mpango wa kando ni Ndoa pia..
Ukisoma kitabu cha Mwanzo 6:1-20 inaonesha jinsi watoto wa Mungu walivyofanya maasi mengi ikiwa ni pamoja na kuoa. "Paulo anasema Msifungiwe NIRA na asiyeamini."
Mwanzo 6:13-20...
Yeye (Mungu) asiyekosea alitoa vipimo vya kujenga SAFINA. Inaitwa SAFINA ya Nuhu kwa sababu; gharama zote zilizotumika zilikuwa za Nuhu.
Mungu wetu ni Mungu asiyekosea, hivyo hata vikosi vyetu vya shule ya Sabato ni mpango wake Yeye asiyekosea.
Nuhu alihubiri miaka 120 lakini wakaokolewa watu 8 tu.
Majanga haya yanayotokea isikukatishe kujenga SAFINA ya kwenda Mbinguni. Ni watu 8 tu hawa ndio waliobakia kama Masalio wa Mungu Kama vile wana wa Mungu watakaookolewa siku za mwisho maana wamedumu kuitii Sauti ya Mungu.
Mpendwa chagua kudumu ndani ya kanisa la Masalio linalodumu kuitii sauti ya Mungu na Amri zake. Chagua kubatizwa leo ili kumkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako.
MUNGU AKUBARIKI SANA.

Comments
Post a Comment